Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge ameupongeza uongozi wa Hospitali ya St.Gaspar Itigi kutokana na huduma Bora za kibingwa wanazozitoa kwa wananchi wa Singida na Mikoa ya jirani.
Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni alipofanya ziara Katika Wilaya ya Itigi Mkoani hapo Katika Hospitali ya St.Gaspar Itigi na kutembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Itagata iliyopo Kijiji Cha Itagata.
Aidha Dkt.Mahenge akijibu hoja maombi ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo yaliyosomwa na Fr Justin Boniface RC amesema Serikali itaendelea kutoa ruzuku kwa wananchi wake Katika sekta ya afya ili waweze kuimarisha Maisha yao.
Amesema pamoja na huduma nzuri na vipimo vinavyopatikana Katika Hospitali hiyo ni vyema kila.mwanachi akapata bima ya afya iliyoboreshwa ili kupata unafuu Lindi wapatapo maradhi.
Ametoa wito kwa madaktari na viongozi hao kuhalikisha huduma hizo zinaendelea kuboreshwa kuongeza mashine nyengine ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kuenda mikoa.mingine kwa ajili ya vipimo alisema Dkt.Mahenge.
Akiwa Hospitalinj hapo Mkuu wa Mkoa alitembelea miundombinu mbalimbali ya Hospitali hiyo pamoja na mashine ya vipimo mbalimbali
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Fr. Justin Bonifasi aliomba Serikali iwafutie deni lenye thamani ya shilingi milioni 333,389,925 linalodaiwa na TRA ombi ambalo RC aliwambia walete ofsini kwake kwa maandishi ili aweze kuguatilia.
Mkurugenzi huyo amesema endapo watalazimika kulipia deni hilo wata athirika kiuchumi na watakao umia zaidi ni wananchi zaidi.
Katika hatua nyingine Dkt.Binilith Mahenge amewataka Viongozi wa Wilaya ya Itigi Mkoani Singida kuangalia upya utaratibu wa kuyagawa mashamba kwa wakulima katika Skimu ya Umwagiliaji ya Itagata Wilayani hapo ili iweze kuwa na Tija katika mkoa.
Maelezo hayo ameyatoa baada ya kutembelea Skimu hiyo na kubaini uwepo wa mashamba makubwa ambayo hayatumiki.
Amesema wapo watu waliohodhi mashamba hayo bila kuyatumia wakati maji yapo ya kutosha huku wakisingizia ubovu wa miundombinu ya Barabara na uwepo wa vichuguu.
Akiongea na wanakiji wa eneo hilo Dkt Mahenge ametaka kuitishwa haraka kwa Mkutano utakao husisha Wakulima wote wa Skimu na Viongozi wa maeneo hayo ili watafakari namna ya kuyagawa mashamba hayo upya kwa wakulima ambao wana utayari.
Aidha amebainisha kwamba Serikali imetoa zaidi ya bilioni 2.1kwa ajili ya utengenezaji wa Skimu hiyo lakini matokeo yake imekuwa ikitumiwa na watu wachache huku ikiendelea kuwa na tija ndogo.
RC Mahenge amewataka Viongozi wa Skimu hiyo kuhakisha msimu unaoanza wa kilimo mashamba yote ya Skimu hiyo yanatumika kulima kilimo cha kibiashara.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.