SERIKALI mkoani Singida, imesema haitomvumilia mtu au watu watakaosambaza taarifa potovu zenyelengo la kukwamisha zoezi la chanjo lililoanza mkoani hapa nalinatarajia kumalizika Oktoba 21 mwaka huu.
Mkuuwa mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, ametoa onyo hilo wakati akizindua kampeni ya chanjo shirikishi ya Surua – Rubella iliyofanyika Oktoba 17, 2019 kimkoa Itigi wilayani Manyoni.
Alisema chanjo ya Surua – Rubella ni chanjo inayolenga kuwakinga watoto dhidi ya upofu, kutokusikia (kiziwi). Mtindio wa ubongo na ulemavu mwingine.
Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni muhimu sana kwani magonjwa hayo hayana tiba.
“Naagiza watendaji wa vitongoji na kata, wasimamie chanjo hii ambayo inalenga watoto wenye umri kuanzia miezi tisa hadi ambao hawajafikisha miaka mitano. Watu watakaopotosha kwa lengo la kukwamisha chanjo hii wakamatwe na wachukuliwehatua stahiki”,
“Ninyi wazazi siyo wageni wa huduma hizi za chanjo. Mmekuwa mkishuhudia watoto wenu wakipata sindano mbili hadi tatu kwa wakati mmoja. Huduma za chanjo ni zakawaida. Jukumu lenu ni kuhakikisha mnawafikisha watoto kwenye vituo vyakutolea chanjo”. amesema
Aidha, Mkuu huyo wa mkoa, amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wa kike wenye umriwa kuanzia mika 14, wanapata chanjo mbili zitakazowakinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.
Alisemakwa mujibu wa wataalamu, maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi, yameenea sana nchini, hivyo ni lazima tuhakikishe tunakuza jamii iliyokingwa kuanziasasa.
Awali, Mganga mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick, alisema jumla yawasichana 12,99 wenye umri kuanzia miaka 14 walipata chanjo ya kwanza dhidi yasaratani ya mlango wa kizazi kati ya Januari hadi Agosti mwaka huu.
Alisema kati ya wasichana hao 6,724, wamefika kukamilisha dozi ya pili ambayo nisawa na asilimia 51.7. Wasichana 6,275 hawakukamilisha dozi hiyo.
“Ikumbukwe kuwa, kinga kamili hupatikana baada ya kukamilisha dozi zote mbili. wananchi watambue kuwa Serikali inawekeza gharama kubwa, ili kuwakinga wasichana hawadhidi ya saratani ya mlango wa kizazi. Hivyo kuna umuhimu mkubwa wazazi kuhakikisha watoto wao, wanapata chanjo zote mbili”,amesisitiza.
Kwa mujibu wa Dkt. Ludovick jumla ya watoto 225,586 wanatarajiwa kupata chanjo yasurua Rubella. Watoto wengine 119,198 wanatarajia kupata chanjo dhidi yaugonjwa wa Polio kwa njia ya sindano.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.