Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Wakuu wa Wilaya waliotambulishwa Mkoani hapo leo kwenda kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ikiwemo migogoro ya ardhi pamoja na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia Wakuu wa Wilaya wanne wa Wilaya ya Iramba, Ikungi, Mkalama na Manyoni katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa walipokuwa wakitambushwa rasmi ambapo aliwaeleza kwamba Mkoa huo una migogoro ya ardhi ambapo mingi ipo Wilaya ya Manyoni.
Amesema namna pekee ya kutatua changamoto hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya viongozi na wananchi na kudhibiti vitendoo vya rushwa ili kuwapatia haki kwa kila anaye stahili.
Aidha RC Serukamba amewataka kusimamia swala la mapato kwa kuwa bado inaonekana uwepo wa mianya ya uvujishaji wa fedha za Serikali, ambapo ameelekeza kufanywa uchunguzi wa kina katika Biashara "services levi" minadani na leseni za biashara kwani huko ndipo penye upotevu.
Wapo wafanya biashara ambao hawatoi stakabadhi wanapofanya mauzo, wengine wanaandika risiti pasipo kuweka "carbon" hivyo kukosekana kwa kumbukumbu wanapo kaguliwa na TRA." alisema
Hata hivyo amewataka Wakuu hao kwenda kusimamia kilimo ili wakulima waendelee kuongeza eneo la kulima huku akibainisha kwamba Mkoa wa Singida umekuwa Mkoa wa pili kwa kuongeza eneo la kilimo ukiondoa Mkoa wa Morogoro.
Akimalizia hotuba yake RC Serukamba amewataka kuhakikisha wanasimamia jukumu la upandaji miti katika kingo za barabara, vyanzo vya maji, mashuleni na majumbani kwa kupitia wanafunzi wanatakiwa kugawiwa miche minne kwa kila mtu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata akizungumza wakati wa hafla ya kuwatambulisha Wakuu wa Wilaya za Halmashauri Mkoani Singida.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson, akitoa salama mara baada ya kutambulishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemilembe Lwota, akitoa salama mara baada ya kutambulishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Joshua Nassari, akitoa salama mara baada ya kutambulishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali, akitoa salama mara baada ya kutambulishwa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili, akitoa salama mara baada ya kutambulishwa.
Picha ya pamoja
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.