• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RC Singida awatembelea wananchi 50 Wanusurika kwa Kula Chakula Kinachodaiwa Kuwa na Sumu

Posted on: September 11th, 2021

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewatembelea wananchi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa huo baada kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu ambapo katika tukio mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 7 amefariki dunia huku watu wengine 50 wakinusurika kifo.

Wakazi hao wa Kata ya Unyambwa kijiji cha Kisasida katika Manispaa ya Singida mkoani Singida walifikishwa hospitalini hapo jana baada ya hali zao kuwa mbaya kutokana na kula chakula kilichoandaliwa katika shughuli za ufunguzi wa Madrasa kijijini hapo.

Dkt. Mahenge amewapongeza madaktari wa Hospitali hiyo kwa jitihada za kuhakikisha wananusuru maisha ya wananchi hao ambapo kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri na kuipongeza Serikali kwa kuweka miundombinu mizuri ya huduma katika sekta ya afya.

Ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali na Dini kuwajibika kikamilifu katika kutoa elimu ya namna ya kuandaa chakula pamoja na kusimamia inapotokea sherehe mbalimbali kwenye maeneo yao ili kuepuka madhara ya namna hiyo.

Kwa mujibu wa Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Banuba Deogratius amesema walipokea jumla ya wagonjwa 50,kati yao Wanawake 34 na Wanaume 16 ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wameanza kuwaruhusu baadhi yao kurudi nyumbani kuendelea na majukumu yao.

Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa amesema wanawashikilia washukiwa 7 walioshiriki kuandaa chakula hicho kwa ajili ya uchunguzi na tayari wamechukua chakula hicho kwa uchunguzi zaidi.

Katika tukio hilo Kamanda amesema mtoto mmoja mwenye umri wa miaka (7) ambaye amefahamika kwa jina la Fahad Masudi amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KILIMO CHA MASHAMBA YA PAMOJA YA KOROSHO, WILAYA YA MANYONI – SINGIDA May 02, 2022
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • SINGIDA INVESTMENT GUIDE February 23, 2021
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2022 - MKOA WA SINGIDA December 24, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Dkt. Mahenge Atangaza Fursa kwa Wawekezaji Mkoani Singida

    May 14, 2022
  • Madiwani Watakiwa kushiriki kikamilifu zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi na Posti Kodi Wilayani Manyoni

    May 11, 2022
  • Taasisi binafsi zatakiwa kuonesha ushirikiano katika uwekaji wa Anwani za Makazi Manispaa ya Singida.

    May 10, 2022
  • Watendaji wa Makiungu, Mungaa Watakiwa kufanya "Data Cleaning" Katika zoezi la uwekaji wa Anwani za Makazi.

    May 09, 2022
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida. Haki Zote Zimehifadhiwa.