• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

“Serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wazawa”- RC Mahenge.

Posted on: September 9th, 2021

Serikali mkoani Singida imesema itaendelea kuwasimamia na kuwaunga mkono wawekezaji wadogo wa ndani ambao wamewekeza katika sekta tofauti mkoani humo kwa sababu wamekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa na kuongeza ajira kwa watanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Singinda Dkt. Binilith Mahenge ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kiwanda cha maziwa cha muwekezaji mdogo kinachofahamika kwa jina la  TAISH Farm kilichopo katika kijiji cha Mtipa mtaa wa mwembe mmoja katika manispaa ya Singida.

Dkt. Mahenge amebainisha kwamba Serikali itaendelea kutoa mazingira wezeshi  kwa wawekezaji ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili .

Aidha amempongeza mkurungezi wa kiwanda hicho Bw. Hassani Tati kwa kusaidia upatikanaji wa soko la maziwa kutoka kwa wafugaji wadogo ambapo hununua lita zaidi ya 70.

Hata hivyo kiwanda hicho kimekuwa kikizalisha ajira kwa watanzania kupitia mnyororo wa thamani ambapo kiwanda kimeajiri watumishi na wengine kupata ajira katika maduka ya kuuzia maziwa hayo. Alisistiza RC.

Akijibu changamoto za ubovu wa barabara, ukosefu wa umeme zilizotajwa na mkurugenzi wa kiwanda hicho, Mkuu wa Mkoa amewaagiza TANROAD na TARURA  kupeleka ofisini kwake  mpago wa utengenezaji wa barabara hiyo inayoingia kiwandani hapo ili washauriane na kuanza utengenezaji mara moja.

Aidha amewataka shirika la umeme TANESCO  kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanafikisha umeme katika eneo hilo la kiwanda ikiwa ni pamoja na vijiji vingine 12  vilivyo ndani ya manispaa ya Singida ili kurahisisha uwekezaji na uboreshwaji wa kiwanda hicho.

Amesema zoezi la upelekaji umeme katika maeneo hayo anaamini litakuwa rahisi kwa kuwa shirika la umeme TANESCO wamepewa Zaidi ya shilingi bilioni tatu (3) ili kusambaza  umeme vijijini  alibainisha Dkt. Mahenge.

Mkuu wa Mkoa amemshauri mwekezaji huyo  kuchukua mkopo benk ili aweze kununua mashine za kisasa kwa ajili ya uongezaji wa thamani ya maziwa  kwa kuwa Serikali itatatua changamoto za barabara pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika.

“Bado una nafasi ya kuongeza uwekezaji na kufanya vizuri zaidi hivyo nakushauri ufungue vituo vidogo vya kukusanyia maziwa  ambapo utakuwa unapima ubora hukohuko, hii itamsaidia mfugaji kutotembea mwendo mrefu na maziwa  yataendelea kuwa salama zaidi”. Alimalizia Mkuu wa Mkoa.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda Bwana Hassani Tati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema kiwanda hicho kwa muda wa miaka mitano kimekuwa kikitengeneza bidha mbalimbali za maziwa zikiwemo mtindi, maziwa fresh na  yogati zenye ladha tofauti.

Amesema maziwa hayo yananunuliwa kwa wafugaji wa Singida na yanauzwa Manyoni, Ikungi, Singida,  Mkalama, Shelui, Igunga, Ikungi na Dodoma

Aidha Bwana Hassani amebainisha kwamba pamoja na changamoto ambazo Serikali imekiri kuzitatua lakini bado kuna changamoto ya upatikanaji wa vifungashio vya bidhaa hiyo ambapo wanalazimika kuviagiza nje ya nchi.

Mwisho aliomba Serikali kutafuta wawekezaji wengine wa vifungashio ili kuachana na uagizaji wa bidhaaa hiyo nje ya nchi.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.