Ukaguzi wa miradi katika Manispaa ya Singida umefanyika leo Tarehe 16 Mei,2025 chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ambapo miradi hiyo inajumuisha miradi iliyopata fedha kutoka Serikali kuu na kutoka katika mapato ya ndani.
Mradi wa Barabara ya Mungumaji inayojengwa na TARURA yenye urefu wa mita 700 iliyopo katika eneo la Majengo.Mradi huu wenye thamani ya Shilingi 659,059,882.25 unajengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu na unatarajiwa kuwekwa Jiwe la Msingi Mwezi Julai katika Mbio za Mwenge.
Majengo ya huduma za Afya mradi unaosimamiwa na Idara ya Afya uliopo eneo la Mandewa linajumuisha jengo la ICU,EMD,na Oxygen Plant mradi ambao unatekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu.
Kadhalika ukaguzi umefanyika katika ujenzi wa Mabwawa ya kutibu Majitaka yakiyopo katika eneo la Mtipa lililogharimu kiasi cha Shilingi 1,730,606,000 fedha kutoka Serikali Kuu.
Mradi wa ujenzi wa Shule ya Amali katika eneo la Unyambwa inayogharimu kiasi cha Shilingi 1,400,000,000 fedha kutoka Serikali Kuu ambayo inatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi katika Mbio za Mwenge Julai.
Pia Jengo jipya la Ofisi za Manispaa lililiofikia asilimia 60 katika ujenzi limekaguliwa huku ujenzi ukiendelea linatarajiwa kukamilika Juni 30,2025.Ujenzi wa jengo hilo unagharimu kiasi cha Shilingi 3,200,000,000 baada ya kupokea fedha kutoka Serikali Kuu.
Katika kuimarisha huduma za afya,ujenzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto Unyamikumbi unaendelea ambapo unatekelezwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa Shilingi 50,000,000
Kikundi cha Vijana kilichopata Mkopo wa Asilimia Kumi kutoka Serikalini,Florida Alluminium and Welding Association Group katika kata ya Majengo kilitembelewa kufahamu maendeleo yake mara baada ya kupata Milioni 15 na kuanzisha biashara yao ya utengenezaji wa Aluminium.
Akizungumza baada ya ukaguzi wa jengo la Halmashauri,Katibu Tawala Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga alishauri umaliziaji wa wakati wa marekebisho madogo yakiyosalia katika ujenzi wa Jengo la Halmashauri sambamba na uwekaji wa samani za Ofisi zenye viwango bora.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Dendego baada ya kukagua soko la vitunguu na eneo ka mnada alitoa maagizo ya kuhakikisha kuwa wanaweka maeneo ya jengo la Hospitali kwa kuhakikisha wanapanda miti na maua kuzunguka maeneo hayo.Kadhalika aliagiza eneo la mnada kusafishwa na kuwa safi kwa matumizi ya wananchi
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.