Mkuu wa Mkoa wa Singida. Peter Serukamba ametoa onyo kwa maafisa ugavi mkoani hapo ambao wamekuwa wakisabisha ucheleweshaji wa miradi inayotekelezwa kwa ‘force Account’ kwa kuweka michakato mirefu ya manunuzi ambayo kwa mujibu wa taratibu za mirad hiyo haihusiki.
Onyo hiyo amelitoa hivi karibuni wakati akikagua miradi ya ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule vilivyopo Wilayani Manyoni Mkoani hapo ambapo kila alipobaini changamoto yoyote kwenye mradi alitajwa afisa manunuzi kwamba anaendelea na michakato ya ununuzi jambo ambalo RC Serukamba amesema sio sahihi.
Amesema miradi inayotumia ‘force account’ huwa zinaundwa kamati tatu ambazo ni kamati ya manunuzi, ya mapokezi na kamati ya ujenzi ambazo kila moja inashughulikia na kazi yake hivyo haikuwa na sababu ya maafisa ugavi kununua, kuingilia au kuratibu michakato ya manunuzi.
"Afisa manunuzi kwenye miradi hii anahusikaje? kuweka michakato ya ununuzi kwenye miradi hii ni kutupotezea muda na kutafuta faida kwa upande wake, kamati zilizoteuliwa ki sheria zinatosha"
RC Serukamba alitembelea miradi minne ambayo ni ujenzi wa wodi mbili na mochwari katika hospitali ya Wilaya hiyo, Kituo cha Afya Sanza, Ujenzi wa shule ya Msingi Nanduka na shule ya msingi Heka ambapo kati ya hiyo ni mradi mmoja tu wa Nanduka ambao hajakutana na changamoto ya ucheleweshaji wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi kama mbao na mabati.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa wodi ya wanawake RC Serukamba ameendelea kusema kwamba hatamuonea aibu yeyote atakayesababisha fedha za miradi kurudi huku akiendelea kusisitizia kwamba atawachukulia hatua watakao onekana kuchelewesha mradi kwa hila zao.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kulia) akisomewa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya Sanza wilayani Manyoni wakati wa ziara hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Sanza wilayani Manyoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (haonekani pichani) wakati akisomewa taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya Sanza.
Ujenzi wa wodi mbili na mochwari katika hospitali ya Wilaya Manyoni ukiendelea
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.