Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka wananchi wa Mkoa huo kushiriki Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano kwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka, upandaji wa miti na kuhakikisha wanashiriki shughuli za ujenzi wa shule zilizopo katika mradi mpya wa boost.
Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao chake na waandishi wa habari mkutano uliofanyika ofisini kwake ambapo amesema kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika shule ya Msingi Minga iliyopo Manispaa ya Singida ambapo watashiriki shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Aidha ameeleza kwamba watumishi pamoja na jamii kwa ujumla watashiriki kufanya usafi maeneo yote ya Mkoa wa Singida hasa katika maeneo ya barabara kuu ya Singida, Mwanza, Ofisi za Serikali na taasisi mbalimbali.
Amesema Mkoa umefanya mahojiano na wazee maarufu wanajua historia ya muungano historia ya Mkoa wa Singida kabla na baada ya muungano ambapo wameielezea jamii umuhimu wa muungano huo na ulivyosaidia katika mambo ya uchumi, siasa na elimu.
Aidha ameeleza kwamba Mkoa utafanya bonanza la Mkoa la michezo ambapo ameeleza kwamba litafanyika tarehe 25 Aprili 2023 katika uwanja wa Bombadia Manispaa ya Singida.
Hata hivyo ameendelea kueleza kwamba wanafunzi wataadhimisha kwa kuandika insha kwa shule za msingi na sekondari.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma taarifa katika kikao chake na waandishi wa habari mkutano uliofanyika ofisini kwake.
Mkutano ukiendelea
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.