Mkoa wa Singida umefanya kikao kazi kilichowakutanisha Waratibu na Viongozi wa Wafanya Biashara Ndogo Ndogo kutoka Halmashauri zote saba, kwa lengo la kuweka mikakati ya kuongeza kasi ya usajili wa wafanyabiashara hao kupitia mfumo wa kidijitali.
Kikao hiki kilichoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Bi Donatila Vedasto kilikusanya Waratibu wa Wafanya Biashara Ndogo Ndogo pamoja na Viongozi wao kutoka Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida.
Lengo kuu lilikua ni kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza kasi ya usajili wa Wafanya Biashara Ndogo Ndogo katika mfumo wa kidijitali. Usajili huu unalenga kuwawezesha kupata vitambulisho rasmi vya ujasiriamali vinavyowatambua katika mifumo ya Serikali.
Kupitia kikao hiki, washiriki walijadili changamoto zilizopo katika utekelezaji wa zoezi la usajili, pamoja na kuazimia hatua za pamoja za kuongeza ufanisi na uwiano wa usajili kulingana na idadi ya wafanyabiashara waliopo.
Mojawapo ya sababu kuu ya kuharakisha usajili ni kuwaunganisha Wafanya Biashara Ndogo Ndogo na fursa ya kupata mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na Benki ya NMB, mikopo ambayo inalenga kuongeza mitaji na kukuza biashara zao kwa njia rasmi, salama na jumuishi
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.