Wataalamu wa Kilimo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wameshauriwa kufanya tathmini katika Skimu ya Umwagiliaji maji ya Itagata yenye ukubwa wa ekari 400 na kuigawa kwa vijana 100 au zaidi wa kata hiyo ili iweze kutumika katika uzalishaji baada ya ushirika wa eneo hilo kushindwa kuiendesha.
Ushauri huo umetolewa leo (Juni 22, 2023) na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, alipo hutubia Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo likiwa na lengo la kujadili namna ya kufunga hoja za ukaguzi (CAG).
Amesema lengo la Skimu hiyo halijafikiwa kwa kuwa wapo baadhi ya watu ambao wameodhi mashamba huku wakilima kidogo jambo ambalo husababisha kupatikana kwa mapato kidogo ya Halmashauri na ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia kilimo.
Aidha ameeleza kwamba namna pekee ya kuhusisha skimu hiyo ni kupitia kwenye ushirika na kuwagawia vijana wa maeneo hayo na kuwawekea utaratibu maalumu ambao utawafanya walime na wakopeshwe mbolea na mbengu ambazo watazirudisha wakivuna.
"Nashauri watafutwe vijana 100 wa kike na kiume wapewe mashamba hayo kila mmoja heka 4 Halmashauri muwakopeshe mbegu na mbolea nina hakika watalipia tozo za Tume ya Umwagiliaji mtapata kodi na uchumi wa eneo hilo utabadilika" alisema Serukamba.
RC Serukamba amesisitiza kwamba kama zoezi hilo halitafanyika skimu hiyo itaendelea kuharibika na kupoteza fedha za Serikali.
Amesema watu kutoka nje ya eneo hilo wamekuwa wakichukua mashamba makubwa ndani ya skimu hiyo huku wakilima kidogo na sehemu kubwa kuyakodisha jambo ambalo amesema halina tija kwa Halmashauri.
Awali Afisa Kilimo Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo Mkinguzi Mgalula, alisema skimu hiyo yenye ukubwa wa ekari 400 ilijengewa miundombinu ya umwagiliaji ikiwemo bwawa lenye uwezo ujazo wa Lita Milioni moja na laki moja na mifereji yeye urefu wa Mita 550 na ilitegemewa kutumiwa na wakulima 200 lakini mpaka sasa wanao faidika ni wachache.
Hata hivyo amesema wamepokea maelekezo ya RC na muda si mrefu wataanza utekeleza wa agizo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemilembe Lwota, akizungumza wakati wa kikao hicho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.