• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SOKO JIPYA LA VITUNGUU,WAFANYABIASHARA KUPINDUA MEZA KIUCHUMI

Posted on: October 20th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ameagiza viongozi wa Halmashauri kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa Soko jipya la Vitunguu lililopo Kititimo, ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa na kwa viwango vya juu.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika eneo jipya la ujenzi wa soko hilo, Mhe. Dendego amesema Serikali ina dhamira njema ya kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuhakikisha Singida inakuwa kitovu cha biashara ya vitunguu nchini.

“Singida tunakwenda kipindua meza, tunakwenda kuweka historia ya kipekee kwa mradi huu mkubwa na wa kipekee. Hii ni moja ya sababu ya kwenda kuuweka mkoa wa Singida kwenye ramani ya kuwa Jiji la Singida. Na hili linawezekana kwa utekelezaji wa miradi hii mikubwa. Tutegemee mwezi Septemba 2026 kukata keki ya mafanikio baada ya kukamilika kwa mradi huu wa TACTIC,” amesema Mhe. Dendego.


Kadhalika, amemtaka mkandarasi kuhakikisha maeneo muhimu yanazingatiwa katika ujenzi wa soko hilo ikiwemo maeneo ya zahanati, michezo, mapumziko, kumbi za mikutano pamoja na maeneo ya sekta binafsi kuwekeza katika huduma za kifedha. Amesisitiza pia kazi kufanyika kwa ubora ili gharama kubwa za ujenzi ziendane na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.



Awali, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, aliwataka wajumbe wa kikao hicho kufikisha salamu za Serikali kwa wananchi na wafanyabiasharawa Soko la Vitunguu juu ya nia njema ya kuhamishia soko hilo maeneo mapya. Amesema eneo hilo jipya litakuwa rafiki zaidi kwa wafanyabiashara na litakidhi idadi kubwa ya wajasiriamali kuliko soko la sasa, hivyo kuongeza faida maradufu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Soko la Vitunguu-Misuna, Bw. Iddi Mwanja, amesema wafanyabiashara wamepokea kwa mikono miwili na kwa furaha kubwa mradi wa soko jipya kwa kuwa utawanufaisha kwa kiasi kikubwa sambamba na kufanya kazi zao kwa uhuru katika mazingira bora na rafiki kwa wote.

“Serikali yetu tunaiamini, tuiache ifanye kazi yake. Tutafuata utaratibu tunaopewa kwa sababu ina nia njema kwetu sisi wananchi,” amesema Bw. Mwanja.

Naye Katibu wa Soko la Vitunguu, Bw. Mshujaa Salum Mwacha, amesema hawana hofu kwani viongozi wamekuwa wakiwasikiliza na kuwashirikisha vizuri katika kila hatua ya maandalizi ya mradi huo. Ameongeza kuwa wamefurahia kuona soko jipya limewapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalum sambamba na akinamama wanaonyonyesha.

Mkandarasi anayehusika na ujenzi huo ameahidi kuhakikisha ujenzi unakuwa wa viwango vya juu na unakamilika kwa wakati, akisisitiza kuwa wananchi wa Singida wajiandae kupokea soko zuri la kisasa lenye mazingira rafiki kwa kazi zao za kila siku.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Katibu Tawala wa Wilaya, Wajumbe wa Soko la Vitunguu, Afisa Mazingira, Afisa Maendeleo ya Jamii, Mtaalam wa Ardhi, wataalam kutoka TARURA, wakandarasi na wadau wengine wa maendeleo.

Mradi huu wa ujenzi wa Soko jipya la Vitunguu unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya biashara mkoani Singida kwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara, kuongeza mapato ya Serikali, kutoa ajira kwa wananchi, pamoja na kuongeza thamani ya zao la vitunguu linalolimwa kwa wingi katika mkoa huo. Soko hilo pia litauwa na miundombinu rafiki kwa watu wote, likiwa na huduma muhimu kama zahanati, maeneo ya mapumziko, michezo na huduma za kifedha, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Singida na kuchangia utekelezaji wa mpango wa kuifanya Singida kuwa Jiji la kisasa.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • SOKO JIPYA LA VITUNGUU,WAFANYABIASHARA KUPINDUA MEZA KIUCHUMI

    October 20, 2025
  • WANANCHI WAHAKIKISHIWA USALAMA WAO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

    October 18, 2025
  • MABINGWA WA CECAFA WAKARIBISHWA NYUMBANI BAADA YA USHINDI MNONO

    October 05, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WAWASILI SINGIDA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

    October 06, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.