Mifumo ya TEHAMA imetajwa kuongeza makusanyo ya fedha za Serikali katika Wilaya ya Singida kutoka shilingi bilioni 1.98 mwaka 2014/15 mpaka shilingi bilioni 4.01 mwaka 2021 ambapo Wilaya ina mashine 280 za kukusanyia mapato.
Akiongea Julai 22, 2021 Katika hospitali ya St. Carolus Mtinko wakati wa uzinduzi wa mradi wa matumizi mbalimbali ya TEHAMA uliozinduliwa na mbio za Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili amesema matumizi ya Mifumo ni muhimu katika kuokoa muda na kuinua uchumi wa watu na Taifa kwa ujumla.
Amesema kwamba, kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2021 “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; Itumike kwa usahihi na uwajibikaji” imeakisi hali halisi ya miradi ya wilayani hapo ambapo mifumo imekuwa ikitumika kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Mhe. Mhandisi Muragili amebainisha kwamba mifumo hiyo imechangia Utumishi wa umma kuwa rahisi ikilinganishwa na awali ambapo kwa sasa imekuwa ikitumika katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii na utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na watumishi.
Naye Afisa TEHAMA Bw. Joseph Micka Joseph amezitaja baadhi ya mifumo inayotumika kuwa ni mfumo wa bajeti (Planrep), mfumo wa taarifa za Watumishi na Mishahara (Lowson –HCMIS), ukusanyaji wa mapato (LGRCIS), utunzaji wa taarifa za wagojwa (GoT- HoMIS) mfumo wa kiuhasibu katika utoaji wa huduma (FFRS), Taarifa za shule (SIS) mfumo wa vibali vya kusafiri nje ya nchi ( SAFARI), mfumo wa malipo (EPICOR- MUSE) na mfumo wa barua pepe.
Kwa upande mwingine Mwenge wa Uhuru 2021 umezindua mradi wa lishe bora katika kata ya Ilongero ambapo wilaya imejivunia kupunguza idadi ya watoto wenye utapiamlo kutoka watoto 22,854 kwa mwaka 2019/2020 hadi kufikia 18,215 mwaka 2021 kwa watoto chini ya miaka 5.
Aidha Afisa lishe wa mradi huo Bi. Asha Mahami amesisitiza kwamba uhamasishaji wa matumizi ya lishe bora yamefanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano 20 na vikao 32 vya wazazi na walezi katika vijiji na mitaa 61 na kata 31, lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto anapata lishe bora kwa siku 1,000 za mwanzo.
Aidha miradi mingine ni malaria uliopo kata ya Mtinko mradi wa maji katika shule ya sekondari ya Itaja, ujenzi wa tenk la maji , Maabara na jengo la uthibiti wa ubora wa elimu lililopo Manispaa ya Singida.
Mwenge wa Uhuru 2021 ukiwa Unawaka, Unang'ara na Kumelemeta ndani ya Wilaya ya Singida katika Miradi mbalimbali ya maendeleo
Baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Singida wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Maji wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2021
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Lt. Josephine Paul Mwambashi (kulia) akipokea risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili wakati wa sherehe za Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, katika uwanja wa shule ya msingi Ukombozi mjini Singida Julai 22, 2021
HABARI PICHA ZAIDI BONYEZA; singidars.blogspot.com
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.