Watendaji na Maafisa Elimu Kata wametakiwa kuwa wabunifu na kuimarisha usimamizi katika miradi ya Serikali inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Maelezo hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko wakati akiongea na viongozi hao baada ya kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Afisa Tarafa iliyopo Kata na Tarafa ya Nkonko Wilayani Manyoni.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko baada ya kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Afisa Tarafa iliyopo Kata na Tarafa ya Nkonko Wilayani Manyoni.
RAS huyo ameeleza kwamba watendaji wanayo nafasi ya kuhimiza wananchi kujitolea nguvu kazi katika kusaidia shughuli za maendeleo ikiwemo ufatuaji wa tofali kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo vya shule na usombaji wa mchanga na vifusi.
Amesema ni vizuri kuishirikisha jamii katika miradi mbalimbali ili kusaidia upatikanaji na Ujenzi wa vyoo katika mashule ambayo yana upungufu wa matundu ya vyoo katika Kata hizo.
Mwaluko amewahimiza Maafisa Elimu kuhakikisha wanasimamia mashule pamoja na miundombinu yake ikiwemo ujenzi wa vyoo kwa maeneo ambayo yanachangamoto ili wanafunzi wapate utulivu.
Akitolea mfano wa shule ya Msingi Chikola ambayo ilikuwa haina vyoo alisema siku chache zilizopita alitembelea shule hiyo ambapo alimtaka Mkuu wa shule, Afisa Elimu Kata pamoja na Mtendaji kuhakikisha shule inakuwa na vyoo katika kipindi cha wiki mbili tofauti na hivyo angeifunga ambapo mpaka sasa tayari ujenzi wa choo hicho umeshakamilika.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA
Muonekano wa Nyumba ya Afisa Tarafa ya Kilimatinde Wilayani Manyoni
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.