• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

UFAULU DARASA LA SABA WAONGEZEKA MKOA WA SINGIDA NA WANAFUNZI WOTE WALIOFAULU WAMECHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2019

Posted on: December 17th, 2018

MKOA wa Singida umefanikiwa kujikwamua kutoka nafasi ya mwisho mwaka jana hadi nafasi ya 14 mwaka huu kwenye Mtihani wa kuhitimu Darasa la Saba Kitaifa.

Afisa Elimu wa mkoa wa Singida, Nelasi Mulungu alikiambia Kikao cha Uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2019 mjini hapa kuwa mkoa umeweza kunyakua nafasi hiyo baada ya kufaulisha jumla ya wanafunzi 20,617 ikiwa ni sawa asilimia 75.21.

Alisema kuwa kiwango hicho cha ufaulu ni ongezeko la asilimia 13.21 ikilinganishwa na asilimia 61.97 mwaka jana.

Mwl. Mulungu alieleza kuwa jumla ya wanafunzi 27,412, kati yao wavulana 12,668 na wasichana 14,741 walifanya Mtihani, hivyo watahiniwa zaidi ya 6,700 hawakuweza kufaulu Mtihani huo.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu huyo, Halmashauri iliyofanya vizuri zaidi kati ya saba zilizopo mkoa wa Singida ni Itigi kwa asilimia 84.56 huku ikishika nafasi ya 50 Kitaifa, Singida Manispaa inafuatia kwa asilimia 81.95, Halmashauri ya wilaya ya Singida 81.02, Manyoni 77.34, Ikungi (74.77), Iramba (74.73) na Mkalama ufaulu wa asilimia 57.87 na hivyo kushika nafasi ya 7 kati ya halmashauri 7 kimkoa.

Mwl Mulungu alisema licha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kushika nafasi ya mwisho kimkoa lakini ufaulu wake umeongezeka hadi kufikia asilimia 57 ikilinganishwa na mwaka jana ilipokuwa na asilimia 37.08 jambo ambalo linapaswa kujivunia.

Alisema kuwa Wanafunzi waliofanya Mtihani mwaka huu ni asilimia 75.24 tu ya idadi yote ya wanafunzi 36,427 waliandikishwa Darasa la Kwanza 2012, hali inayoonesha wazi kuwa zaidi ya wanafunzi 9,000 waliacha shule njiani kwa sababu mbali mbali, ikiwemo kufariki, mimba, utoro na uhamisho.

Alitaja baadhi ya mikakati ya kuendelea kuinua kiwango cha ufaulu kimkoa kuwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha kuwa walimu wanafanya maandalizi ya ufundishaji na kufundisha kikamilifu. Pia mikakati mingine ni kuandaa mitihani miwili ya utamilifu kwa wanafunzi wa darasa la Saba na la Nne. Aidha, kila mwezi kutakuwa na uwasilishaji wa upimaji kwa madarasa hayo kutoka katika kila Halmashauri kwa kila shule.

Kwaupande wake, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Mhandisi Paskasi Muragili, aliutaka uongozi wa mkoa na wadau wa elimu kwa ujumla kuunganisha nguvu pamoja ili kuisaidia Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ili iweze kufanya vyema zaidi hapo mwakani.

Mhe. Mhandisi Muragili alisema kuwa, halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inahitaji nguvu ya Mkoa ili kumaliza changamoto mbalimbali zinazosababisha wasifanye vizuri zaidi katika matokea ya mitihani ya shule za msingi ikiwemo mazingira yaliyoizunguka Halmashauri ya Wilaya hiyo iliyogawanywa kutoka wilaya mama ya Iramba.

Alizitaja miongoni mwa changamoto hizo ni uhaba wa Walimu, mwamko duni kwa baadhi ya familia, jamii ya wafugaji, umasikini na hata jamii ya Wahadzabe kuwemo katika wilaya hiyo, hivyo kuhitajika nguvu ya ziada ili kuikwamua.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Singida alisema ingawa hiyo siyo wilaya yake kiutawala, lakini iwapo itasaidiwa kimkakati basi huenda ikasaidia kuchangia mkoa mzima wa Singida kufanya vyema zaidi na hata kuwa miongoni mwa mikoa mitano bora katika ufaulu wa matokeo ya darasa la saba hapo mwakani.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT.SAMIA WABISHA HODI SINGIDA

    April 23, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.