Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo ametembelea eneo linalojengwa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu lililopo Mtipa katika Wilaya ya Singida ili kuona eneo hilo na kusikiliza mipango ya Ujenzi kutoka kwa Mkandandarasi.
Akiongea akiwa katika eneo hilo RC Mahenge amesema uwanja huo ukikamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Singida kwa kuwa watatumia michezo kama sehemu ya ajira na kipato.
RC amebainisha kwamba kutokana na ukweli kwamba Singida ni katikati ya nchi uwanja huo utaweza kutumiwa na mikoa ya jirani lakini hata wananchi kutoka mikoa hiyo wanaweza kuja kuangalia mpira.
Aidha RC ameagiza Mkandarasi huyo kukutana na Shirika la ugavi wa Umeme Tanesco na Idara ya maji ili waweze kubaliana kila mmoja atakapoweka miundombinu yake ambayo itarahisisha Ujenzi huo kwenda kwa kasi kubwa.
Hata hivyo amebainisha kwamba uwanja huo utakapokamilika utasaidi kuongeza uwekezaji eneo hilo na kuongeza kipato kwa wanachi kupitia Biashara za hoteli na huduma mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akamtaka Mkandarasi kuandaa wasilisho kwa viongozi ili kuona mchoro ili waweze kuwashawishi wafanyabiashara Kuwekeza maeneo hayo kwa ajili ya kurahisisha huduma nyingine.
DC Muragili akaendelea kumhamasisha Mkandarasi kujitahidi ili uwanja huo uweze kutumika kabla ya kuisha mwaka huu kwa kuwa kutasaida kufungua fursa nyingine za ndani.
Naye Mkandandarasi wa uwanja huo kutoka Kampuni ya Senga senga civil & building company amesema eneo hilo lina ukubwa wa ekari zaidi ya 10 ambapo kwa sasa eneo lishafanyiwa usafi na wanajipanga kusawazisha kabla ya kujenga hosteli katika kwa ajili ya wageni.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.