• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WADAU WA UKAGUZI WAKUTANA SINGIDA KUJADILI NAMNA BORA KUEPUKA HATI CHAFU, ZENYE MASHAKA.

Posted on: September 17th, 2021

WASHAURI wa mambo ya fedha leo wamekutana katika ukumbi wa ofisi za ukaguzi wa hesabu za serikali (NAO) Mkoani Singida kujadili namna ya kutatua changamoto zinazosababisha upatikanaji wa hati chafu au zenye mashaka kulingana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa Fedha 2019/20 katika baadhi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Imeelezwa pamoja na mambo mengine, lengo la kikao hicho ni kukubaliana na kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia wakaguzi na wakaguliwa kutekeleza wajibu wa kisheria kwa namna ambayo itaongeza tija na kuboresha utendaji.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi hicho, Katibu Mkuu TAMISEMI Profesa Riziki Shemdoe alisema matokeo ya ukaguzi huo hayakuwa ya kuridhisha kutokana na mwenendo usioridhisha wa Hati za Ukaguzi zilizopatikana ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliotangulia wa 2018/19.

"Kumekuwa na poromoko la halmashauri kupata hati safi na hii haikubaliki. Haiwezekani kuwe na poromoko la hati safi kutoka halmashauri 176 mwaka 2018/19 hadi halmashauri 124 mwaka 2019/20...nahitaji kikao hiki kije na mkakati madhubuti na maazimio yatakayosaidia kuleta maboresho stahiki," alisema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, halmashauri zilizopata Hati Zenye Shaka ziliongezeka kutoka 9 mwaka 2018/19 hadi halmashauri 53 mwaka 2019/20, huku 8 zikijikuta zinapata Hati Chafu.

Alisisitiza kwa kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia Waweka Hazina na Maafisa Masuuli kuwa makini katika kipindi hiki wanapokwenda kufunga vitabu, kwa kuhakikisha zinajiepusha na aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi yasiyofaa ya fedha za umma ili kuepuka hati chafu na zile zenye mashaka.

"Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki ambacho namuona mwakilishi wa Ofisi ya CAG, Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Maafisa Masuuli na wadau wengine mliopo tuhakikishe tunajadili kwa kina changamoto zote zilizojitokeza na kuhakikisha hazijirudii," alisema.

Aidha, Prof. Shemdoe alisisitiza baada ya kikao hicho kilichofadhiliwa na USAID kupitia Mradi wa PS3+, Ofisi ya Rais-TAMISEMI itakuwa tayari kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa na kuratibu utekelezaji wa yale yote yatakayopaswa kutekelezwa na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika muktadha wa maboresho ya huduma bora kwa wananchi.

Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Divisheni ya Serikali za Mitaa, Benjamin Mashauri akizungumza wakati wa mkutano

Kwa upande wake, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Divisheni ya Serikali za Mitaa, Benjamin Mashauri, alibainisha sababu kubwa ya ongezeko la hati chafu na zile zenye mashaka kuwa kubwa ni changamoto kwenye eneo la uandaaji wa Hesabu.

Pia Mashauri alisema eneo lingine linalopelekea hali hiyo ni kwenye mapato ambayo pamoja na mambo mengine, mengine hukusanywa lakini hayapelekwi benki wala kwenye mifumo stahiki.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni kwamba taarifa za kwenye vitabu haziendani na taarifa halisi za mapato yanayokusanywa. Hali inayopelekea kiasi kikubwa cha matumizi ya Fedha za Umma kujikuta zikifanyiwa matumizi bila ya kuwa na viambatanisho stahiki.

"Vilevile kuna masuala ya changamoto za matumizi ya mifumo ya kisasa katika uandaaji wa hesabu kulingana na Kanuni za Mfumo wa Kimataifa za uandaaji wa Hesabu za Taasisi za Umma., huko nyuma tulikuwa na mfumo wa Epicor sasa ni Muce, hivi vyote visipozingatiwa hupelekea matokeo ya uzalishaji huu wa hati chafu na zenye mashaka," alisema Mashauri.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.