Katika kuadhimisha miaka 30 ya Mamlaka ya Chuo cha Ufundi Stadi(VETA) Mkoa wa Singida umeazimia kuanzisha program maalumu kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza shule za Msingi na Sekondari kusoma VETA kwa wale watakaohitaji ili waongeze ujuzi.
Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego wakati akifunga maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa VETA .
Mhe.Dendego amesema kuwa wataandaa program maalumu kwa ajili ya wanaomaliza darasa la saba, Kidato cha Nne na kidato cha Sita wanapomaliza wakati wanasubiria majibu wapate ujuzi kwa miezi sita katika chuo cha VETA.
Katika hatua nyingine amewasisitiza wananchi kuiunga mkono VETA kwa kazi nzuri wanayoifanya,Pia amewashauri kutumia fursa hiyo kwa kuwatambua na kuagiza watu wenye ujuzi waendelee kuhudumia wanafunzi kwa kuwapa ajira ndani ya Halmashauri kwa lengo la kuendelea kukuza vyuo hivyo na taaluma za wanafunzi wote wanaonufaika na elimu hiyo.
Pia ametumia fursa hiyo kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya katika miradi ya Maendeleo hasa katika kuongeza idadi ya vyuo vya VETA huku kukiwa na vyuo vitano vya VETA kwa mkoa wa Singida.
Sambamba na hilo,amepongeza chuo cha VETA wakiongozwa na Wakurugenzi kwani vijana wanasoma na kupata ujuzi akisema kuwa VETA ni muhimu sana kwani inawezesha idadi kubwa ya wanufaika kuwa na ujuzi ambao unawawezesha kujiajiri.
Awali, Alitembelea ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida, unaosimamiwa na mafundi waliopitia VETA, na kuwapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa ujuzi mkubwa huku akiwasisitizia kuendelea kujifunza zaidi kuongeza ujuzi wao .
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.