• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Wakandarasi Mkoani Singida waaswa kukamilisha kwa wakati miradi ya ujenzi

Posted on: November 23rd, 2022

Wakandarasi waliofanikiwa kupata tenda ya Ujenzi wa barabara Mkoani Singida wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi kwa wakati kama walivyokubaliana katika mikataba yao ya kazi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa utiaji saini baina ya Wakandarasi hao na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Aidha Serukamba  amewataka Wakandarasi hao kuondoa kero za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Mkoa huo kwa kuhakikisha wanajenga Barabara zenye ubora wa hali ya juu na kuzikamilisha kwa wakati ili wananchi waweze kurahisisha maisha yao.

Hata hivyo RC Serukamba amewataka TARURA kusimamia kikamilifu Wakandarasi hao kwa kuwa Serikali imetoa fedha zaidi ya Bilioni 21.2 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara za Mijini na Vijijini na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.

Aidha RC Serukamba amewaagiza TARURA, TANROAD na RUWASA Mkoani hapo kuanza utaratibu wa kufanya tathmini baada ya kumaliza taratibu za kutoa tenda kwa Wakandarasi ili kupima mchakato ulivyokwenda na kuona kama kulikuwa na makosa yaliyotolewa awali.

Hata hivyo ameeleza kwamba ni lazima taarifa hizo ziwe za wazi ambapo walioshindanishwa wanaweza kuona utaratibu ulivyokwenda mpaka kupatikana washindi.

RC amesema utaratibu huo utasaidia kuondoa rushwa katika mchakato mzima wa kupata Wakandarasi wenye sifa na ubora na kusaidia kuona makosa yaliyofanyika awali ambayo hayataweza kurudiwa katika kipindi kingine.

"Tukimaliza manunuzi yote kwa mwaka TARURA, TANROAD na RUWASA muwe na checklist inayoonesha tenda zilizofanyika na mchakato ulivyokwenda moja kumpatia Mkandarasi, rushwa haiondolewi ki babe bali inaondolewa kwa mfumo" alisema RC

Awali akitoa taarifa yake Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David amesema TARURA katika mwaka wa fedha wamepanga kutengeneza Barabara zenye urefu wa km 944 na kujenga jumla ya madaraja na vivuko 72.

Aidha Mhandisi Tembo ameeleza kwamba TARURA Singida wamejipanga kufanya matengenezo ya kawaida ya Barabara kwa urefu wa Km 483 na matengenezo ya sehemu korofi zenye urefu wa km 224 pamoja na matengenezo ya muda maalum yenye urefu wa km 237.

Pamoja na mambo mengine TARURA itatekeleza majukumu ya utenegenezaji wa madaraja na vivuko 72 na Ujenzi wa barabara za kiwango cha lami chenye urefu wa km 5.1 na km 550 ambazo zitajengwa kwa kiwango cha changarawe na km 388.9 kiwango cha udongo.

Aidha Mhandisi Tembo amesema utekelezaji wa Ujenzi wa barabara umefikia asilimia 30.

Kwa niaba ya Wakandarasi walioweza kupata tenda hizo Siamen Kimaro Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanlite Labour Based Contractor amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kumalizi kwa wakati huku akiahidi ubora mkubwa katika kazi waliyopata.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa utiaji saini baina ya Wakandarasi na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.