Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ametoa rai kwa wakulima wilayani Mkalama kujisajili katika mfumo ili waweze kupata mbegu na mbolea za ruzuku.
Ameitoa kauli hiyo Leo, Desemba 16, 2024 katika kijiji cha Ilunda Kata ya Ilunda wakati wa hafla ya kumkabidhi Mshindi wa tuzo Mkulima Bora Kitaifa wa Maonesho ya Nane nane 2024 yaliyofanyika katika viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma
“Serikali ilianza na mbolea na sasa imeanza kutoa ruzuku kwenye mbegu za Mahindi na Alizeti,wito wangu kwenu nendeni mkajisali ili muweze kupata mbegu kwa bei nafuu” Mhe. Machali
Akizungumzia suala la utunzaji wa Mazingira, Mhe. Moses Machali amewataka wakazi wa kijiji cha Ilunda kupanda miti katika kupambana na uharibifu wa mazingira akiwasihi kupanda miti mingi ambayo itakua chanzo Cha mvua za kutosha .
"Tukiwa na miti mingi tutapata mvua za kutosha na tutakuwa tumetunza mazingira” Mhe. Machali
Aidha Mhe. Moses Machali amewakumbusha wakazi wa Ilunda na Mkalama ujumla kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa Amani, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujilinda dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Suzana Mwakiro amesema tuzo iliyotolewa ni chachu ya Kila mmoja kupambana kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa sehemu ya kumuinua Kila mmoja katika nyanja ya kiuchumi na hata kijamii pia Kwa kuwa chanzo Cha kuwapatia wananchi chakula Cha kutosha.
"Kilimo ni uti wa mgongo wa watanzania,hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunafaidi Matunda yake Kwa kuhakikisha tunazitukua vema fursa za mbegu na mbolea za ruzuku tunazopewa na Serikali Kwa mavuno mengi na Bora"amesema Suzana.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.