Wakulima Wilayani Ikungi wamelalamikiwa kwa kitendo cha kulima katika maeneo mengi ya hifadhi ya Barabara jambo ambalo linakwamisha jitihada za matengenezo ya Barabara hasa nyakati hizi za mvua.
Lalamiko hilo limetolewa hivi karibuni na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ikungi Mhandisi Ally Number wakati wa majadiliano yaliyofanyika katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika Halmashauri hiyo.
Mhandisi Ally amebainisha kwamba wakulima wengi Katika kata za Sepuka Makilawa Ihanja Nduru Mkiwa na Mwaru wamelima Katika hifadhi ya Barabara Jambo ambalo litasababisha kucheleweshewa kwa kazi za matengenezo ya Barabara.
Sambamba na hilo Mhandisi Ally amesema bado wafugaji wa Wilaya hiyo wanaendelea kupitisha mifugo Barabarani Jambo ambalo kunasababisha uharibifu mkubwa wa barabara hasa kipindi hiki cha mvua hivyo kuiomba jamii kuacha tabia hiyo kwa kuwa Barabara hizo hutumia fedha nyingi za Serikali katika kukarabatiwa.
Awali Baraza la Madiwani lilipitisha bajeti ya Tarura Ikungi kwa mwaka 2022/23 kiasi cha Bilioni 4.72 Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ally Juma Mwanga alisema endapo zikitumika kama mipango ilivyowekwa wanategemea maeneo mengi yatafunguliwa na barabara nyingi zitapitika.
Mwenyekiti huyo amesema Kata zote za Ikungi zitaguswa katika bajeti hiyo ambayo yapo maeneo ya kata hizo yatajengwa madaraja kata nyingine Barabara zitafunguliwa mpya wakati maeneo mengine yakijengwa madaraja makubwa na madogo.
Hata hivyo Mhandisi Ally alitoa ufafanuzi kwamba fedha hizo zilizotengwa zitatumika katika utenegenezaji wa barabara Madara na nyingine kwa ajili ya usimamizi ambapo jumla ya KM 156 na madaraja 20 na makalavati 61 vitajengwa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.