Wakuu wa Idara za Kilimo Mkoani Singida wamepewa muda wiki mbili kuhakikisha wanaandikisha wakulima katika daftari la kilimo kufikia asilimia 85 au zaidi Kwa lengo la kuhakikisha wakulima wanapata huduma ya mbegu na mbolea za ruzuku kuelekea Msimu mpya wa kilimo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego wakati wa kikao Cha mrejesho wa wadau sekta ya kilimo kutathimini uandikishaji wa wakulima ambapo halmashauri zote za Mkoani Singida ziliwasilisha utekelezaji wa uandikishaji huo umefikia hatua gani ili kurahisisha upatikanaji wa mbegu na mbolea kuelekea Msimu wa kilimo ulionza sasa.
Akizungumza katika kikao hicho,Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amesisitiza utendaji WA kazi Kwa bidii Kwa vitendo zaidi kuliko mikakati ya maneno isiyo ya vitendo akiwataka kutoka mijini na kuwafuata wakulima maeneo Yao mpaka vijijini wanapoishi ili kuwa rahisi kuwapata na kuwapatia elimu ya kilimo wakati wa kuwasajili.
"Msirudi nyuma,rudini kazini mkawe sababu ya wakulima wetu kufanya vizuri kwasababu tunataka kuona kilimo chenye tija kufikia Disemba 31 iwe asilimia mia moja.Tujitume wenyewe na tusisubiri maelekezo kutoka Kwa viongozi wa juu Bali tuende mpaka vijijini walipo tuwafikie Kwa urahisi na tuwape elimu ya kilimo juu ya mbegu na mbolea za ruzuku."amesema RC Dendego
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama,Mhe.Moses Machali akizungumza katika kikao hicho amesema ni wazi kuwa wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wakulima wanajisajili hivyo amewashauri wakurugenzi kuvutumia vizuri vyama vya ushirika na AMCOS kurahisisha ufikiwaji mzuri na wa uhakika k a mkulima kuhudumiwa huku akisisitiza matumizi ya mfumo WA uandikishaji kiteknolojia katika simu ili kuwafikia wakulima wengi Kwa wakati mfupi.
Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Kilimo na uzalishaji Bw Starnslaus Choaji amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi Yale yote yaliyoazimiwa katika kikao hicho na kuwataka wakuu wa Idara ya kilimo kukutana na kutatua changamoto zote zitakazojitokeza na kuonekana kikwazo katika kufikia malengo yaliyowekwa.
Pia amesema kuwa ni vema kuwahisha mbegu Kwa wakulima kwani mvua zinatarajiwa kuwa chini ya kiwango mwaka huu na kuainisha mawakala mbali mbali ambao wapo tayari kufanya nao kazi Kwa bei rafiki Kwa wakulima kumudu gharama na upatikanaji wa haraka.
Akizungumza baada ya kikao,Bw.Eli Jackson Muna kutoka Wilaya ya Ikungi Kata ya Ntutu amesema wakulima wanategemea mbegu na mbolea za ruzuku kuwahishwa mapema katika maeneo Yao ili kuweza kuzipata na kupanda mapema Kutokana na Hali ya hewa iliyopo huku akiomba mzunguko wa kupata huduma hiyo kuwa mfupi Ili kumfikia mkulima Kwa haraka zaidi.
Katika Mkoa wa Singida mpaka sasa wakulima 108,506 sawa na asilimia 34 wameandikishwa kati ya malengo ya wakulima 316,684 yaliyowekwa huku upatikanaji wa mbegu za alizeti ukiwa Tani 105 kati ya Tani hitajika 1206 na mahindi yakihitajika Tani 316,684.Mbolea mahitaji ni Tani 15,834 huku ikitumika Tani 3,501.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.