Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe.Halima Dendego amewaaga wanamichezo wa timu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo inakwenda kushiriki michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) ambayo inatarajiwa kuanza siku ya kesho (Septemba 18,2024) Mkoani Morogoro.
Akiwaaga wanamichezo hao katika hafla fupi ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Dendego amesema kuwa Mkoa una mategemeo makubwa sana na wanamichezo hao kwani wanaibeba bendera ya Mkoa wa Singida na wanapaswa kuipeperusha vema kwa kurejea na ushindi mnono.
“Tunategemea muende mkashinde na mkatuwakilishe vema katika michezo yote na nidhamu kwa ujumla mkatuwakilishe vema mkoa wa Singida” Alisema Mheshimiwa Dendego.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatuma Mganga, akizungumza katika hafla hiyo amesema kuwa maandalizi makubwa yamekwishafanyika kuhakikisha mahitaji yote muhimu kwa wanamichezo hao yamepatikana kwa wakati hivyo ni jukumu lao wasasa kuhakikisha kuwa wanakwenda kuuwakilisha Mkoa vema kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo.
“Tunalo deni kubwa la kuheshimisha Mkoa wa Singida kwa kurudisha nishani nyumbani na kuleta ushindi katika Mkoa wa Singida”Sura ya Singida itaonekana kupitia nyinyi katiaka nidhamu,kujituma,tabia njema na utendaji wenu”Alisema Dkt.Fatuma Mganga.
Fedrick Ndahani miongoni mwa wachezaji na kiongozi wa Timu hiyo inayosafiri kuelekea Morogoro,amesema maandalizi yao ni mazuri na wanatarajia kufanya vizuri kwani wana hari na maandalizi ya kutosha hivo wanakwenda kupambana na kuhakikisha wanarejea na nishani.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kujumuisha watumishi mbali mbali wa serikali,ambapo mwaka huu timu hiyo ya michezo ina jumla ya wanamichezo 30,wanaume 18 na wanawake 12,na kiongozi wa msafara ambapo watashiriki michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu,mpira wa pete,riadha,kurusha tufe, na kucheza karata.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.