MKUU wa Mkoa Singida Dk. Binilith Mahenge amewataka wananchi wa mkoa huo kuchukua tahadhari kwa watu wasiowafahamu wanaofika kwenye maaeneo yao na kuwatilia mashaka.
Mahenge alitoa ombi hilo aliposimama kwa muda kutoa pole kwa wafiwa wa Iddi Hassan (25) mkazi wa Iguguno wilayani Mkalama mwendesha bodaboda ambaye aliuawa kwa chomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni na tumboni na mtu asiyejulikana ambaye alimkodi.
Dkt. Mahenge akizungumza jana na wananchi wa eneo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo aliwaomba wachukue tahadhari kwa kujilinda, kutoa taarifa na kuwa waangalifu kwenye maeneo yao wanayoishi.
Akitolea mfano moja ya tukio lililotokea hivi karibuni Kata ya Nduguti wilayani humo ambapo mtu mmoja aliyejitambusha kuwa amefika katika kata hiyo kama muajiriwa wa Jeshi la Polisi ambaye alipanga katika nyumba moja ya kulala wageni akiwa na mwanamke aliyedai ni mke wake.
Alisema mtu huyu alikuwa akimtumia mwendesha bodaboda mmoja kumpeleka maeneo tofautitofauti na baada ya kuona amekwisha mzoea wakati wakinywa chai alimwambie amuachie pikipiki yake ili aende kuripoti kituo cha polisi kuhusu kuanza kazi ambapo alimruhusu kuondoka na pikipiki yake na kutokomea nayo kusikojulikana na walipoenda nyumba ya kulala wageni walimkuta na huyo mwanamke aliyedai ni mke wake amekwisha ondoka.
"Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha watu wote waliofanya tukio hilo watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria" alisema Mahenge.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikulu ambacho alikuwa akiishi kijana huyo Christina Lema alisema wamesikitishwa sana na tukio hilo kwani marehemu alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote na alikuwa akishirikiana na waendesha bodaboda wenzake kwenye shughuli zao.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama akitoa salamu za pole kwa wafiwa waliofikwa na msiba huo
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kumsikiliza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge pindi alipokatisha ziara yake kwa muda mchache ili kuwapa mkoa wa pole kwa kuondokewa na kijana wao mpendwa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.