Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameagiza Serikali za Vijijini Wilayani Mkalama kuhakikisha wanaondoa uonevu unaofanywa dhidi ya Wanawake Wilayani hapo ambao wamekuwa wakinyanyaswa na kunyang'anywa ardhi zao.
Kauli hiyo ameitoa leo akiwa katika Kijiji cha Nkalakala alipokuwa akisikiliza na kutatua kero za hapo kwa hapo kwa Wananchi wa Wilaya ya Mkalama ambapo wanawake wengi wajane walilamikia kunyanyaswa na wanaume ambao wamekuwa wakiwanyang'anya ardhi zao jambo ambalo limesababisha kuyumba kwa maisha yao.
RC Serukamba amesema amesikitishwa kuona Wilaya ya Mkalama kuwa na kawaida ya kuwanyanyasa wanawake ambapo ameeleza kwamba hayupo tayari kuona hali hiyo ikiendelea.
Hata hivyo RC Serukamba ametoa agizo kwa Serikali za vijiji kuhakisha wanawake wanalindwa na unyanayaswaji huo unakomeshwa na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaoendeleza tabia hiyo.
"Wanawake Mkalama wanaonewa sana tafadhali Serikali za vijiji iwasaidie ili tukomeshe hali hii, DC naomba hili tulisimamie kwa nguvu zote na wote wanapofanya vitendo hivyo kunyang'anya ardhi za watu wapate ujumbe kwamba hatutawaacha salama". Alisema Serukamba.
Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya Askari ambao wanatumika kunyanyasa watu wanyonge kwamba wakati wao umefika hakuna atakayebaki Mkalama akiendelea kuchafua sifa nzuri ya Jeshi la Polisi.
Amesema kesi za wanawake hao na bàadhi ya wanaume ambao wameonekana kudhulimiwa mali zao ambapo maelezo yanaonesha kesi wanashindwa katika ngazi zote za mabaraza ya ardhi lakini haki wanaonekana kupewa wenye uwezo wa kifedha hivyo RC akalazimika kutoa maagizo kuanzia ngazi ya DC mpaka Serikali ya vijiji kushughulika swala hilo.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na wananchi wa Mkalama wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali akizungumza na wananchi wa Mkalama wakati wa mkutano huo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.