Manispaa ya Singida imetakiwa kuongeza usimamizi na kubaini vyanzo vipya vya mapato vitakavyo saidia kuendesha miradi mbalimbali ambayo inachelewa kukamilika kutokana na Uhaba wa fedha.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge alipokuwa akihutubia Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo lililokutana leo kujadili hoja za ukaguzi Mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwenge Mjini hapo .
RC Mahenge amesema kwamba Halmashauri hiyo ina vyanzo vingi vya mapato ambavyo havijasimamiwa vizuri na endapo usimamizi utakuwa mzuri mapato yangeongezeka kwa kiasi kikubwa.
"Fanyeni tathmini ya vyanzo vyenu vya mapato mjiridhishe muone uwezo wake na kiwango mnachopata vinaendana? Nina amini vyanzo vya mapato Kama vituo vya Afya na standi vina uwezo wa kutoa mapato makubwa havijasimamiwa ipasavyo" Alisema RC Mahenge.
Aidha amewataka kutumia mamlaka na vyombo walivyonavyo kukusanya mapato ili kukabiliana na wateja ambao wanakwepa kulipa kodi ya Serikali.
Hata hivyo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuwa na hoja chache za ukaguzi ambazo zinatokana na sera na bàadhi yake kutokana na mikopo ya vikundi.
Hata hivyo RC ametoa angalizo kwa Madiwani pamoja na wataalamu wa maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanafanya tathmini ya mkopaji kabla ya kumkopesha ikiwa ni pamoja na elimu ya ujasiriamali na namna ya kutunza fedha.
Awali akimkaribisha Mkuu huyo Mstahiki Meya Yagi Kyaratu amesema wapo tayari kutekeleza maagizo hayo huku akieleza kwamba tayari wameshaanza kubaini vyanzo vingine vya mapato ikiwemo Ujenzi wa maegesho ya magari kutokana na uwekezaji utakao anza hivi karibuni wa Mradi wa Umeme wa upepo .
Amesema wametenga bajeti kwa ajili ya kutengeneza Mazingira mazuri ya fukwe za ziwa Kindai na Singidani Kama sehemu ya mapumziko ambayo yatatumika pia kuingizia mapato Halmashauri kwa namna tofauti.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.