Mafunzo ya wataalamu wa afya na viongozi mbalimbali wametakiwa kusambaza elimu ya chanjo ya UVIKO 19 katika vituo mbalimbali vinavyotoa chanjo na kwenye mikusanyiko ya watu ili kusaidia kupunguza athari za ugonjwa huo.
Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo ya Siku mbili yaliyofanyika mkoani Singida na kuwahusisha Waganga wakuu wa Wilaya, Maafisa habari na baadhi ya wawakilishi kutoka wizara mbalimbali, Mganga Mkuu wa Mkoa, Victorin Ludovick amesema kumalizika kwa mafunzo hayo ndio mwanzo wa kutoa elimu kwa watoa chanjo na wananchi kwa ujumla.
Amesema elimu waliyopata wakufunzi hao wataenda kuwafundisha wengine kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka Vijijini
Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorin Ludovick akisisitiza jambo wakati wa mafunzo. (Katika) Mwakilishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dinah Atinda na (kulia) Mshauri wa Ugavi kutoka shirika la JSI wanaoshirikiana na wizara ya Afya kupitia idara ya chanjo.
Dkt.Ludovick amesema elimu waliyopata imetoa muongozo wa utoaji wa elimu sehemu mbalimbali ikiwemo minadani na kwenye masoko na sehemu zenye watu wengi.
Mafunzo yamefanya zoezi la utoaji wa elimu ya chanjo kuwa jepesi kwakuwa wataalamu wengi walishapata uzoefu mkubwa kwenye mambo ya utoaji wa chanzo. Alisema Mganga Mkuu wa Serikali.
"Mazoezi kama haya tushayafanya sana kwa hiyo naamini tunaenda kutekeleza tulichojifunza na nategemea kuona matokeo makubwa" alisistiza Dkt. Ludovick.
Pamoja na mafunzo hayo Dkt Victorine amesema mafunzo hayo yatumike kubuni njia mbadala ya kuwafikia wananchi ili kuwaelimisha na kuhamasisha chanjo kwa kila mtu.
Amebainisha kwamba njia nyingine ni kuwatumia viongozi wa dini ili wafikishe ujumbe kwa waumini wao juu ya umujimu wa kupata chanjo na kuondoa imani potofu kwa jamii dhidi ya chanjo ya UVIKO 19
Mwakilishi wa OR - TAMISEMI, Dinah Atinda akisisitiza jambo wakati wa mafunzo
Awali Mwakilishi wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dinah Atinda amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya na pia viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili waweze kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya UVIKO-19 .
Amesema Mpango Jamii Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI na unaendelea kutekelezwa nchi nzima.
Hata hivyo amebainisha lengo la mafunzo hayo kuwa ni kuwajengea uwezo watoa huduma za afya , viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huu.
Mafunzo yakiendelea, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Singida Victorin Ludovick
Afisa Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya - TAMISEMI, Mpango wa Taifa wa chanjo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa Watendaji (walio kaa) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kumaliza mafunzo kuhusu Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa wakufunzi na wadau wa afya mkoani Singida. Septemba 23 - 24/2021
Kwa habari picha zaidi bonyeza singidars.blogspot.com
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.