Hafla ya kuwatunza vyeti watumishi na waajiri hodari katika Mkoa wa Singida imefanyika leo Mei 2,2025 katika uwanja wa Bombadia likihusisha watumishi kutoka katika halmashauri zote za mkoa wa Singida
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,amewashukuru viongozi wote walioshiriki kutoa ushirikiano katika maandalizi yote ya Meimosi Taifa mpaka pale jambo lilipokamilika wakiongozwa na menejimenti ya Mkoa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa , Menejimenti ya TUCTA, viongozi wa Chama cha mapinduzi,vijana wa hamasa,na wananchi kwa ujumla kufanikisha shughuli hiyo.
"Shukran za dhati zimwendee Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jambo jema la kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa asilimia 35 hakika amewatia moyo wafanyakazi na kuwafanya waendelee kujituma zaidi."amesema Mhe.Dendego
Pia amesisitiza kuwa Mkoa wa Singida ni sehemu nzuri sana ya kupokea wageni hivyo ni vyema kwa wafanyakazi wote kushirikiana kwa umoja na nguvu ya mshikamano itasogeza Mkoa mbele kimaendeleo.
Naye Katibu tawala mkoa wa Singida amewaasa wafanyakazi mkoani songea kufanya kazi kwa bidii zaidi kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake vyema kulingana na majukumu yake yanavyomhitaji ili kutoa matokeo mazuri zaiildi katika sekta mbalimbali mtumishi anafanya kazi.
Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Singida ametoa pongezi kubwa kwa wafanyakazi wa Mkoa wa Sungura kwa ushirikiano wao wote waliouonyesha kabla na hata baada ya sherehe za Mei Mosi.Pia amezishukuru kamati mbalimbali zilizohusika katika maandalizi ya sherehe za Meimosi kwa kushiriki pamoja katika kuandaa kikamilifu shughuli mbalimbali za Meimosi kwa ukamilifu
Kwa niaba ya wafanyakazi wote , Mwenyekiti wa TUCTA mkoa amesema kuwa wamepokea kwa moyo mkunjufu ongezeko la mshahara wa wafanyakazi alioahidi kuwaongezea wafanyakazi kwa ongezeko la asilimia 35 litakaloanza mwezi Kikao mwaka huu.
Baada ya hayo Mkuu wa Mkoa alikabidhi zawadi mbalimbali kwa watumishi hodari waliofanya vema katika kazi zao kwa vitengo mbalimbali na kufanikisha mafanikio katika sekta mbalimbali wakiwemo watumishi na waajiri.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.