Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amesisitiza maadili katika maeneo ya kazi kwa kutoa maagizo ya utendaji Bora wa kazi kwa watumishi pamoja na usimamizi bora wa kazi kwa viongozi wa idara na vitengo.
Ameyasema hayo leo hii wakati akifungua kikao cha kujadili mapitio ya bajeti kwa mwaka 2025/26 kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Mhe.Dendego Amesisitiza Viongozi wa idara,vitengo na sekta mbalimbali kuhakikisha wanawajibika kwa kuwaongoza vema waliopo chini yao kwa kutoa maamuzi sahihi na kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira yenye furaha na mazingira bora ya utendaji kazi ambayo yatawafanya kufanya kazi kwa kujiamini na kwa weledi ambayo yataleta matokeo chanya katika utendaji wa kazi.
"Tutimize wajibu kwa kuzingatia haki,wajibu na sheria, changamoto katika Shemu za kazi zipo,tuwe watulivu na wasikivu kwani sisi ni vioo katika jamii hivyo maisha yetu yawaguse wale tunaowaongoza".amesema Mhe.Dendego
Pia amesisitiza nidhamu ya watumishi katika kazi kwa kuwa kioo kwa jamii na wale wanaowaongoza kwa kuhakikisha wanavaa mavazi yanayostahili kazini,aina za misuko,viatu na mengine mengi.
Akizungumzia kuhusu suala la nidhamu kwa watumishi kazini,Katibu Tawala wa Mkoa Daktari Fatuma Mganga amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi kwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali huku akikumbusha watumishi kubwa na haiba ya kuwahi kazini ili kutekeleza majukumu yao kwa wakati muafaka.
Katibu Tawala msaidizi sehemu ya Rasilimali watu Bw.Pancras Stephen amezungumzia suala la ukiukwaji wa maadili kwa watumishi kama sifa mbaya kwa watumishi huku akisema mikakati imekwishawekwa kwa ajili ya kuhakikisha tabia zisizofaa kimaadili kwa watumishi zinazooneshwa ili kurejea katika mstari ulio sahihi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka katika vyama vya wafanyakazi ngazi za halmashauri,wilaya na ngazi ya Mkoa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.