Katika kuhakikisha viongozi wanafanya kazi zao Kwa uadilifu na utawala Bora,Madiwani,wakuu wa divisheni na vitengo,wenyeviti wa vijiji,Mitaa na vitongoji katika Wilaya ya Ikungi na Halmashauri ya Singida wamepatiwa Mafunzo Kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi ili kuwa daraja zuri katika kuwaunganisha wananchi na Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Justice L.Kijazi amefungua mafunzo ya kuboresha utendaji kazi kwa madiwani na wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mafunzo hayo yameanza tarehe 16 Disemba, 2024 huku yakitarajiwa kuendelea mpaka tarehe 20 Disemba, 2024 ambapo Halmashauri imeandaa mafunzo ya ujazaji tamko la maadili kwa viongozi kufuatia matakwa mapya ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma ya ujazaji wa tamko la rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kwa njia ya mfumo kwa mujibu wa sheria.
"Tumealika viongozi kutoka taasisi mbalimbali ili kutoa mada kuhusu uboreshaji utendaji kazi wetu hivyo tutakuwa na mada kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na tamko la rasilimali na madeni na masuala ya serikali za mitaa" amezungumza Kijazi
Mkurugenzi Mtendaji ameongeza na kusema kuwa mwisho wa kujaza Tamko la maadili ni tarehe 31 Disemba, 2024.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe katika mafunzo hayo wameishukuru Halmashauri kwa kutenga bajeti kwa ajili ya mafunzo hayo kwani yanaenda kuwa chachu katika utendaji kazi katika maeneo yao.
Lengo la mafunzo hayo ya siku 5 nii kuwawezesha viongozi hao kujifunza maswala ya utawala bora kwa maslahi mapana ya wananchi wa wilaya ya Ikungi na mkoa wa Singida kwa ujumla.
Kwa upande mwingine Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji kutoka katika halmashauri ya Singida wamepatiwa mafunzo ya Uongozi kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi katika maswala ya uongozi ili kuleta Maendeleo kwa wananchi na kuisaidia Serikali yanayofanyika Kwa siku mbili Disemba 18 na 19,2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ilongero.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI),yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri na kutolewa na wawezeshaji kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Bw.Shabani Mongomongo amewapongeza wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwaongoza wananchi akiwasihi kusimamia misingi ya uongozi pasipo kuingiliana katika utendaji kazi.Sambamba na hilo,ametoa Pongezi kwa Chuo Cha Hombolo kwa kukubali kutoa mafunzo hayo.
Jumla ya wenyeviti wa vijiji 84 na wenyeviti wa vitongoji 435 wanatarajiwa kupata mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa siku mbili.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.