WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Singida ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na uwekaji wa Mawe ya Msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa leo Septemba 30, 2019 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema ziara hiyo ataianza Oktoba 4, 2019 hadi Octoba 6, 2019 na Oktoba 7, 2019 atafungua rasmi maonesho ya Pili ya SIDO Kitaifa mkoani Singida.
Amesema katika ziara hiyo pia, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa (MB) atazungumza na Wananchi pamoja na Watumishi katika mikutano ya hadhara katika kila Wilaya na halmashauri zote za mkoa wa Singida.
” Maonesho haya yatafanyika sanjari na maadhimisho ya wiki ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani Singida kuanzia Oktoba 10 hadi 16 mwaka huu katika Viwanja vya Bombadier”. Dkt. Nchimbi.
Amesema kufanyika maonesho hayo mkoani Singida ni fursa kwa wananchi wa mkoa wa Singida ambao unakuwa kiuchumi kwa kasi kutokana na shughuli za kilimo, ufugaji, biashara na viwanda.
Pia amesema Serikali ya mkoa wa Singida unajivunia kwa kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa maonesho hayo Kitaifa na hii itawapa hamasa kubwa wananchi katika kuanzisha viwanda vidogo vya usindikaji kutokana na mazao yanayolimwa mkoani hapa.
Dkt. Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kupokea ugeni huo na kushiriki katika maonesho hayo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.