Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa WA Singida leo tarehe 28,aNovemba 2024 wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na ugonjwa wa Afya ya akili kwa Watumishi wa Umma mahali pa kazi yaluyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuanzia saa tatu kamili asubuhi.
Akiwasilisha mada kuhusu VVU na UKIMWI,Dr. Said Mgeleka ambae ni Meneja wa Mradi kutoka USAID AFYA YANGU mkoa wa Singida, ametoa mada kuhusu hali ya Maambukizi wa VVU na UKIMWI kwa,uwiano wa wagonjwa kijiografia,umri, Jinsia na Hali ya Ndoa, katika Mkoa wa Singida.
Kuhusu Maambukizi ya VVU kwa Jinsia Amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa jinsia ya kiume imekuwa nyuma katika kupima VVU NA UKIMWI kwani kati ya jumla ya wateja 27,678 waliopo kwenye Huduma za Matibabu; wanaume ni ni 8,581 asilimia 31% pekee huku wanawake wakiwa 19,097
"Kundi linaloongoza Kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI ni watu waliopo katika ndoa sababu kuu ikiwa ni kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja huku kata ya Mandewa na Misuna ikitajwa kuongoza Kwa idadi ya maambukizi" amesema Dr.Mgeleka.
Naye Dkt.Lewis Rwegayula,ambaye ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singidaa amewasilisha mada kuhusu tatizo la Ugonjwa wa Afya ya Akili akianisha sababu,dalili na matibabu ya afya ya akili huku akiwaasa watumishi kutumia muda vizuri kwa kuhakikisha wanamaliza majukumu yao Kwa wakati husika ili kuweza kuyamudu vema mazingira ya kazini na baada ya kazi,Pia kuyatambua mahitaji ya viongozi wao na kuyatekeleza vema ili kuepusha migogoro kazini itakayoweza kuwasababishia tatizo la afya ya akili kwa lengo la kuwa na matokeo mazuri katika kazi.
"Ni vema pia Kwa viongozi kuzitambua vema tabia za wasaidizi wao Ili kufahamu vyema namna gani watawaongoza na kuwasimamia katika utendaji wao wa kazi,pia Kila mmoja ayatambue mapungufu yake na kuyafanyia kazi ili kutokuwa sababu Kwa wengine kupata tatizo la afya ya akili".alisema Dkt Lewis
Pia amewasihi watumishi kuepuka kutumia dawa ambazo hawajaelekezwa na Daktari kwani nazo huchangia tatizo la Afya ya Akili.
Akizungumza Kwa niaba ya Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe,Dkt.Shilla Mwashiuya amewaasa watumishi kuwashauri wenzao Wenye tatizo au dalili za afya ya akili ndani na nje ya ofisi Kwa kuwatia moyo wahusika na kuwasaidia pale inapowezekana na sio kuwavunja moyo na kuzidi kuwakatisha tamaa inayozidisha uwezekano wa kupata tatizo la Afya ya Akili.
Katibu Tawala WA Mkoa wa Singida,Daktari Fatuma Mganga akizungumza baada ya kuwasilishwa Kwa mada hizo amesema ni wakati sasa wa kuamua kunadilika kitqbia Kwa Kila mmoja kuhakikisha anajiepusha na mazingira yote yenye kuweza kusababisha maambukizi ya VVU huku akisisitiza watumishi kuwa na uthubutu wa kupima afya zao katika magonjwa ya kuambukiza na Yale yasiyoambukiza ili kuzifahamu Hali zao vema.
Kuhusu tatizo la Afya ya Akili amesema ni vema watumishi kutumia muda wao mwingi katika shuhuli za kujiingizia kipato baada ya kazi za ofisini ili kupunguza wimbi la watu Wenye tatizo la Afya ya Akili mara baada ya kustaafu akisisitiza matumizi Sahihi ya fedha na kutunza akiba Kwa manufaa Sahihi ya baadae.
"Tukapime afya zetu Kwa kupima magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza,Pia ni vema kufanya mazoezi ya viungo mara Kwa mara ili kuuweka mwili mbali na magonjwa"alisema Daktari Mganga.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.